DR. AGGREY: MGHANA MAHIRI ALIYEACHA HISTORIA TANZANIA HADI "KUPEWA" MTAA JIJINI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DR. AGGREY: MGHANA MAHIRI ALIYEACHA HISTORIA TANZANIA HADI "KUPEWA" MTAA JIJINI DAR

 DR.JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY, aliyezaliwa mwaka 1875 na kufariki takribani miaka 100 iliyopita, ni Mghana ambaye kamwe hatasahaulika katika historia ya nchi yetu, ingawa takriban 90% ya Wabongo hawajawahi hata kumsikia!.
DR. AGGREY alikuwa ni Mwalimu mahiri aliyeheshimika duniani kote. Tarehe 15.5.1895, akiwa Mwalimu-kijana wa miaka 20 tu, alifanya mtihani pamoja na waalimu wenzake wengine 119 kutoka mikoa yote nchini Ghana uliotungwa Uingereza. Dr. AGGREY aliibuka kinara ambapo alitunukiwa cheti na Malkia kilichoandikwa- "This Certificate of Distinction, qualifies you, without further examination, to teach in any school in any British colony". Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika wa kwanza  kutunukiwa tuzo hiyo na Malkia!.
DR. AGGREY, kutokana na weledi wake wa kipekee, aliteuliwa kuwa mjumbe wa "Phelps-Stokes Fund Commission" iliyoundwa kuangalia namna kuwaendeleza Waafrika kielimu. Tume hiyo iliundwa kutokana na Mmarekani Bi. CAROLYINE PHELPS STOKES, aliyefariki 1909,  kuacha kitita cha fe... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More