DRC YAPATA WAZIRI MKUU, MOISE KATUMBI AREJEA NYUMBANI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DRC YAPATA WAZIRI MKUU, MOISE KATUMBI AREJEA NYUMBANI

DRC CONGO
Raisi wa DRC Felix Tshisekedi (kulia) akisalimiana na waziri mkuu wake Prof Ilunga 
Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu hatimaye Rais Felix Tshekedi wa Congo DRC amemteua waziri mkuu mpya.
Waziri mkuu huyo ni professor Ilunga kutoka chama cha Rais Kabila chenye wabunge wengi.
Professor Ilunga ambaye hakutarajiwa kushika nafasi hiyo anapaswa kuunda serikali ambayo mawaziri 80% watakuwa kutoka muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Kabila FCC. Chama cha Tshekedi kinatarajiwa kupata mawaziri asilimia 20 kwa kuwa kina idadi ndogo ya wabunge.
Pia mwanasiasa maarufu aliyehitilafiana na raisi aliyemaliza muda wake, Joseph Kabila, Bwana Moise Katumbi amerejea nchini Congo DRC jana baada ya kuishi uhamishoni miaka mitatu. Kurejea kwake kunatarajiwa kubadilisha sura ya siasa za Congo na huenda akajumishwa serikalini.
Katumbi ndiye mmiliki wa timu ya TP Mazembe. ... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More