DStv sasa kurusha Serie A- kifurushi cha Bomba! - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DStv sasa kurusha Serie A- kifurushi cha Bomba!

Siku chache tu kabla ya kuanza kwa moja ya ligi maarufu Duniani – Ligi kuu ya Italia Serie A, MultiChoice imetangaza neema ya burudani kwa wateja wake kwa kuweka michezo yote 380 ya ligi hiyo katika kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba ambacho hulipiwa shilling 19,000 tu kwa mwezi.
Kama hiyo haitoshi, DStv pia itaonyesha mechi zote 380 za ligi ya Hispania – La Liga katika kifurushi hicho cha bomba huku mechi 108 za ligi kuu ya uingereza (EPL) nazo zikionyeshwa katika kifurushi hicho cha chini kabisa.
“Kama ilivyo ada, sisi DStv kila uchao tunahakikisha kuwa tunamfikishia mtanzania burudani popote alipo na kwa gharama nafuu. Hii ndiyo sababu tumeamua kuiweka ligi hii maarufu katika kifurushi chetu cha Bomba kinachopatikana kwa shilingi 19,000 tu kwa mwezi” amekaririwa Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria.
“Tunatambua kuwa ligi ya Italia ni moja ya ligi zenye mvuto mkubwa ulimwenguni na kama kawaida kwa kupitia DStv, tunawafanya watanzania kuwa sehemu ya ulimweng... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More