Dulla Makabila Amuanika Mpenzi Wake Mpya - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dulla Makabila Amuanika Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa singeli nchini Abdallah Ahmed maarufu kama Dulla Makabila amemuanika hadharani kwa mara ya kwanza mpenzi wake aliyemtambulisha kwa Jina la Maiya Abdul.


Global Publishers wanaripoti kuwa Wawili hawa walinaswa ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo msanii wa filamu za maigizo nchini, Yvone Cherry ‘Monalisa’ alikuwa akizindua mpango wa kuwasaidia wasichana kufikia malengo yao kwenye tasnia ya filamu uitwao, Mona ACT.


Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Dulla alibanwa kuhusu Mrembo huyo ambapo alifunguka na kusema yule ndio mchumba wake na wanategemea kufunga ndoa siku za mbeleni.Huyu ni mchumba wangu anaitwa Maiya na hapa nimefika kwani tuna malengo mengi ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa Mungu akipenda”.Huyu ni mwanamke wa kwanza ambaye ameonekana hadharani na Dulla Makabila tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake Msanii wa Bongo movie Husna Sajent.


The post Dulla Makabila Amuanika Mpenzi Wake Mpya appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More