Dully Sykes Ataja Sababu Za Kumficha Mpenzi Wake - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dully Sykes Ataja Sababu Za Kumficha Mpenzi Wake

Msanii mkpngwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Dully Sykes amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kumuanika hadharani mwanamke ambaye yupo naye kwenye mahusiano kutokana na somo alilolipata siku za nyuma.


Dully amesema kamwe hawezi kumuonyesha mwanamke ambaye hajamuoa kwenye jamii kwa sababu ameshajifunza mengi sana kupitia wasanii wenzake waliothubutu kuonesha wanawake walio nao kwenye uhusiano.


Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari nchini, Dully amesema kuwa kwanza kabisa hana mwanamke kwa sasa lakini kama akimpata atafaidi sana kwani mambo ya kidunia mengi kayaacha kwa sababu hakuna ambalo hajalifanya.Hakuna kitu kibaya kama unatoka na mwanamke unaachana naye anaenda kutembea na rafiki yako ni kitu kibaya mno na cha fedhea sana, hivyo nitamuweka wazi mke wangu, sio msichana tu ambaye wakati wowote unaweza kuachana naye”. 


 


The post Dully Sykes Ataja Sababu Za Kumficha Mpenzi Wake appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More