Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ‘syllabus’ ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo.

 Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka alisema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

“Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kod... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More