EMIRATES WAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

EMIRATES WAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJANa Said Mwishehe, Globu ya jamii. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer amesisitiza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wanaosafiri na ndege zao katika mataifa mbalimbali duniani.
Pia amezungumzia fursa zilizopo kutokana na uwepo wa safari za ndege zinazofanywa na Emirates kati ya Tanzania na nchi nyingine ikiwemo ya usafirishaji mizigo ya kibiashara kutoka Dar es Salaam ambako kumekuwa kituo kikubwa cha kibiashara kwa Afrika Mashariki.
Alfajeer amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika mazungumzo yaliyolenga kujenga uhusiano kati yake na vyombo vya habari kuhusu masuala ya kibashara na maisha.
“Emirates nia yetu ni kuendelea kuhakikisha wateja wetu wanakuwa wenye thamani bora kadri inavyowezekana,” amesema.
Hivyo wanaendelea kuwa wabunifu katika kutoa huduma bora zaidi. “Kila siku tumekuwa tukiangalia njia za ubunifu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja ikiwa pamoja na kurahisi safari zao... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More