Emmanuel Mbasha afunguka ishu ya kupata mchumba mpya baada ya kutemana na Flora - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Emmanuel Mbasha afunguka ishu ya kupata mchumba mpya baada ya kutemana na Flora

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania,  Emmanuel Mbasha amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mahusiano yake kama amepata ubavu mpya baada ya kuachana na Flora .Mbasha amesema kuwa kwa sasa yupo single, bado anasubiri mwanamke atakayechaguliwa na Mungu.


“Namuomba Mungu Mimi bado kijana siwezi kusema miaka yote nitaishi peke yangu.  Namuomba Mungu aje anipe mke mwema na sahihi wa kufanya nae maisha na kukamilisha taratibu zote za kiheshima.”amefunguka Mbasha kwenye kipindi cha E-Gospel cha EFM.


“Kwa sasa hivi bado nipo single, Sina mchumba wala Girlfriend, nimeshachoka kuumizwa,”.


Mbasha amefunguka hayo, baada ya tetesi kuwa amepata mchumba mpya, ambaye mara kwa mara amekuwa akimposti kwenye ukurasa wake wa instagram.


The post Emmanuel Mbasha afunguka ishu ya kupata mchumba mpya baada ya kutemana na Flora appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More