England vs Switzerland, kwanini sekunde 25 za mwanzo zitaoneshwa kwa Black & White? - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

England vs Switzerland, kwanini sekunde 25 za mwanzo zitaoneshwa kwa Black & White?

Hii leo timu ya taifa ya Uingereza inacheza mchezo wao mwingine katika michuano ya UEFA Nations League ambapo watakuwa wenyeji dhidi ya Switzerland.


Lakini kuna jambo ambalo sio la kawaida litatokea katika uoneshwaji wa mechi hiyo ambapo sekunde 25 za mwanzo za mechi hiyo zitaoneshwa bila rangi(itakuwa nyeupe na nyeusi).Hii ni katika kusheherekea miaka 25 ya Kick It Out ambayo ni organization inayohusiana na masuala ya usawa katika mchezo wa mpira wa miguu nchini Uingereza.


Chama cha soka nchini Uingereza FA kimesema Kick It Out wamekuwa muhimu sana kwenye soka la nchini humo na wanaamini sekunde 25 za leo zitatosha kuwakumbusha wapenda soka kuhusu shirika hilo.Lakini pia wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza watavaa tshirt zenye nembo ya Kick It Out wakati wa mazoezi huku wakiingia uwanjani kutakuwa na scout 8 ambao wamechaguliwa na Kick It Out kuwawakilisha.


Waingereza watajaribu kuepuka kipigo cha 4 mfululizo hii leo baada ya kupigwa mara mbili kombe la dunia kisha wakafungwa ... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More