ENYIMBA YAIPIGA RAYON 5-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, AL MASRY WAITOA USM ALGER - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ENYIMBA YAIPIGA RAYON 5-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, AL MASRY WAITOA USM ALGER

TIMU ya Enyimba International imeitupa nje Rayon Sport ya Rwanda katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa mabao 5-1 katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Enyimba International mjini Aba, Nigeria. 
Enyimba inakwenda Nusu Fainali kibabe baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na Rayon Sport kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda wiki iliyopita.
Katika mchezo wa jana, mabao ya Enyimba yalifungwa na Stanley Dimgba dakika ya 12, Ikouwem Utin dakika ya 29, Sunday Adetunji dakika ya 48, Joseph Osadiaye dakika ya 60 na Isiaka Oladuntoye dakika ya 80, wakati la Rayon lilifungwa na Bonfilscaleb Bimenyimana dakika ya 24. 

Mechi nyingine za marudiano za Robo Fainali jana, bao pekee la mshambuliaji mkongwe wa umri wa miaka 33, Mouhssine Lajour dakika ya nne liliipa ushindi wa 1-0 Raja Casablanca dhidi ya CARA Brazzaville Uwanja wa Mfalme Mohamed V mjini Casablanca.
Raja inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1, kufuatia kushinda ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More