ERASTO NYONI ATIWA HATIANI KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA NDANDA FC - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ERASTO NYONI ATIWA HATIANI KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA NDANDA FC

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI mkongwe wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni atapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko Hassan Nassoro Maulid wa Ndanda SC katika mechi namba 33 iliyomalizika kwa sare ya 0-0 Septemba 15 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 

Erasto Nyoni (kushoto) akisalimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli 

Wambura amesema tukio la Nyoni, mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, halikuonwa na Mwamuzi wa mechi hiyo ndiyo maana hakuonyeshwa kadi.
Aidha, Wambura amesema Simba wamepewa Onyo Kali kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake katika kikao cha maandalizi ya mechi hiyo na adha... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More