Esma Adai Anajenga Nyumba Ili Kukwepa Aibu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Esma Adai Anajenga Nyumba Ili Kukwepa Aibu

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan amefunguka amefunguka an kuweka wazi nia yake ya kujenga nyumba ili kuondoa aibu hapo mbeleni.


Esma Platnumz ameweka wazi kuwa anaogopa kuaibika kama ambavyo hutokea kwa mastaa wengi wanapotangulia mbele za haki na kukosa mahali pa kuagiwa.


Katika mahojiano yake aliyofanya na Global Publishers, Esma amedai amejifunza kwa mastaa wengi ambao walikuwa wanatamba mjini, lakini walipofariki dunia ndipo maisha yao halisi yakagundulika ikiwemo kutokuwa hata na nyumba wakati enzi za uhai huonekana wakiishi maisha ya kifahari.Naogopa kuaibika ndiyo maana nimenunua kiwanja maeneo ya Madale (Dar), natarajia kuanza kujenga hivi karibuni ili hata nikifa, watu wasipate shida ya mahali hata pa kuagia”.Esma ameachana na mume wake wa miaka kadhaa Petit Man miezi michache iliyopita na kudai hana haraka ya kutafuta mwanaume mwingine kwani yupo busy na kulea watoto wake.


The post Esma Adai Anajenga Nyumba Ili Kukwepa Aibu appeared first ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More