ESPERANCE YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ESPERANCE YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

TIMU ya Esperance ya Tunisia imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Etoile du Sahel, zote za Tunisia usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse.
Bao pekee la Esperance katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Muivory Coast, Fousseny Coulibaly dakika ya 87 akimalizia pasi ya beki mkongwe wa umri wa miaka 31, Mtunisia, Sameh Derbali.
Ushindi huo wa ugenini katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali unaifanya Esperance isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 2-1 Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Olimpiki wa Rade.

Mchezo mwingine wa Robo Fainali leo, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetupwa nje kwa mabao ya ugenini, baada ya Mazembe kulazimishwa sare ya 1-1 na C.D. Primeiro de Agosto Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
Mshambuliaji kinda wa miaka 20 wa DRC, Jackson Muleka aliifungia bao la kuongoza Mazembe mapema tu dakika ya 12, akimalizia pasi ya kiungo Muivory Coast, Christ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More