ETIENNE NDAYIRAGIJE AULA, AKABIDHIWA MIKOBA YA AMUNIKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ETIENNE NDAYIRAGIJE AULA, AKABIDHIWA MIKOBA YA AMUNIKE

Kikao cha Kamati ya dharura cha Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambacho kimekutana leo,kimemtangaza Kocha Mkuu wa Azam Ndayiragije Etienne kuwa Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Etienne,amependekeza benchi lake la ufundi kusaidiwa na kocha wa Coastal Union Juma Mgunda pamoja na kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania Suleiman Matola,ambapo uteuzi huo umezingatia programu maalumu ya kuendeleza makocha wazawa. 
Aliyekuwa kocha Mkuu wa Timu hiyo Emanuel Amunike alisitishiwa mkataba wake baada ya kukubaliana kwa pamoja na TFF mapema wiki hii.
Etieene ataiongoza Taifa stars kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza CHAN wakikabiliana na Kenya Harambee Stars kati ya Julai 24-28 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwenye michuano ya Mataifa Afrika AFCON Taifa Stars walikuwa kundi moja na Kenya na katika mchezo wao wa hatua ya makundi Harambee Stars walishinda 3-2 na wote kuondolewa na Stars wakiambulia alama sifuri, Kenya alama 3... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More