ETO’O AWASILI DAR NA KUMKUMBUSHIA IVO MAPUNDA MACHUNGU YA YOUNDE 2008 STARS NA CAMEROON - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ETO’O AWASILI DAR NA KUMKUMBUSHIA IVO MAPUNDA MACHUNGU YA YOUNDE 2008 STARS NA CAMEROON

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MWANASOKA Bora wa zamani Afrika, Mcameroon Samuel Eto'o leo amekumbushia machungu ya uwanjani kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ivo Mapunda walipokutana mjini Dar es Salaam.  
Eto’o ambaye kwa sasa anamalizia soka yake katika klabu ya Qatar SC, amewasili nchini jioni ya leo kwa shughuli za uzinduzi wa Uwanja wa soka eneo la Coco Beach mjini Dar es Salaam, kabla ya kukutana na Mapunda.
Eto’o alitua mchana wa leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mjini Dar es Salaam na kupokewa na mwenyeji wake, Meneja wa Castle Lager, Pamera Kikuli kabla ya kupelekwa katika hoteli ya Ramada, eneo la Kunduchi mjini hapa.
Gwiji wa Cameroon, Samuel Eto'o (kulia) akiwa na kipa wa zamani wa Taifa Stars, Ivo Mapunda baada ya kukutana tena leo Dar es Salaam

Samuel Eto'o na Ivo Mapunda wakiwa na Meneja wa Castle Lager, Pamera Kikuli (katikati) katika Hotel ya Ramada mjini Dar es Salaam jioni ya leo

Na huko ndiko Eto’o mwenye umri wa miaka 37 alipokutana... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More