Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

Pengine ulikuwa hujui jina BATE ni kifupisho cha Borisov Automobiles and Tractor Electronics, ndio! Nimetaja trekta, FC BATE inamilikiwa na kiwanda cha magari huko nchini Belarus. FC BATE wameshinda taji la Ubingwa wa ligi kuu ya Belarus mara 13 mfululizo, hawa ndio watawakaribisha Arsenal katika uwanja wa Borisov Arena Alhamisi hii majira ya saa 2:55 Usiku.
Mchezo wa Arsenal ni moja kati ya 16 itakayochezwa Usiku wa Alhamisi hii katika hatua ya 32 bora. Michezo ambayo kwa hapa Tanzania itarushwa na kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee kupitia chaneli zao za michezo.
Kwa upande wao Arsenal huenda wakaendelea kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Americk Aubameyang ambaye ni mgonjwa. Hata hivyo Arsenal watajipa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo baada ya kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Huddersfield 2-1 katika ligi kuu ya Uingereza. Itakumbukwa pia msimu uliopita Arsenal waliichapa BATE 4-2 ugenini na kisha 6-0 katika dimba la Emirates, hivyo wataingia uwanja... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More