FAINALI YA MAPINDUZI CUP: Mnyama ‘Simba SC’ achinjwa na Azam FC kisiwani Pemba - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FAINALI YA MAPINDUZI CUP: Mnyama ‘Simba SC’ achinjwa na Azam FC kisiwani Pemba

Mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC na Simba SC umemalizika kwa Mnyama Simba SC kupigwa goli 2-1 katika Uwanja wa  Gombani, kisiwani Pemba.

Azam katika kipindi cha kwanza walipata bao la kwanza kupitia kwa Mudhathir Yahya kunako dakika 43.

Yahya aliachia shuti kali akiwa kwenye eneo D akimalizia pasi ya Ennock Atta ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Simba, Ally Salim na kuwafanya Azam FC.

Kipindi cha pili dakika 64 Simba walipata kona iliyopigwa na Shiza Kichuya, Yusuf Mlipili aliitupia kichwa kichwa safi kilichozaa bao la kusawazisha

Obrey Chirwa ndiye aliyetupia bao la ushindi kwa Azam FC na ndiyo wanakuwa mabingwa wapya mara tatu mfululizo wa kombe hilo kwa mwaka 2019.The post FAINALI YA MAPINDUZI CUP: Mnyama ‘Simba SC’ achinjwa na Azam FC kisiwani Pemba appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More