FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Fainali za mashindano ya vilabu vya kodi zilizoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zimefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Shule za Sekondari zilizoibuka na ushindi na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano hayo.

Fainali hizo zilizofunguliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilifanyika jana katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Shule ya Sekondari St. Joseph iliibuka mshindi wa kwanza kati ya shule 28 za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuzawadiwa runinga, kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti.

Shule ya Sekondari Tumbi imeshika nafasi ya pili ambayo ilijinyakulia kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Dar es Salaam ambayo ilipata ngao, kompyuta ya mezani, saa ya ukutani na cheti.

Kwa upande wa uwasili... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More