FAMILIA YAMLILIA MWANAFUNZI WA KITANZANIA ALIYEFARIKI MAREKANI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FAMILIA YAMLILIA MWANAFUNZI WA KITANZANIA ALIYEFARIKI MAREKANI

"Tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa. Alipenda sana masuala ya utabibu, na alienda Marekani kupata mafunzo na kutekeleza ndoto zake," imeeleza familia ya kijana Allen Buberwa, ambaye amefariki nchini Marekani mwanzoni mwa wiki.Buberwa, 22, ambaye alikuwa ni mwanafunzi unesi katika chou cha North Arkansas College alifikwa na umauti baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye mto Buffalo. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 jioni jimboni Arkansas, Marekani.

Taarifa rasmi zinaeleza kuwa, Buberwa na rafiki zake watatu walienda mtoni huku wawili kati yao wakiingia majini na kuogelea. Buberwa pamoja na kijana mwengine walisalia ukingoni mwa mto.

Ghafla Buberwa aliteleza na kutumbukia mtoni na kushindwa kujinasua, kijana mwenzie aliyekuwa naye pia alijirusha ili amuokoe lakini pia akanasa. Rafiki zao wawili waliotangulia mtoni walijitahidi kuwaokoa lakini Buberwa alisalia chini ya maji.

Vikosi vya uokozi viliupata mwili wake majira ya saa tano usiku wa siku hiyo hiyo ya tukio.

"Kwa ujumla tum... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More