FAO: ZAIDI YA WATOTO MILIONI 108 WANATUMIKISHWA DUNIANI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FAO: ZAIDI YA WATOTO MILIONI 108 WANATUMIKISHWA DUNIANI


Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema bado watoto wanaendelea kutumikishwa kwenye sekta ya kilimo ulimwenguni kote na hivyo kuathiri uwezo wao wa kustawi na kujinasua kwenye umaskini pindi wanapokuwa watu wazima. Assumpta Massoi na ripoti kamili. 
FAO inasema kuwa duniani kote watoto milioni 108 wa kike na wa kiume wanatumikishwa ambapo asilimia 70 wanafanya kazi kwenye sekta za kilimo, ufugaji, misitu, uvuvi na ufugaji wa samaki.
Idadi hiyo, kwa mujibu wa FAO imeongezeka kwa watoto milioni 10 tangu mwaka 2012, licha ya jitihada za Umoja wa Mataifa za kutokomeza utumikishaji watoto kwenye sekta hizo.
Ariane Genthon ambaye anahusiska na programu ya FAO ya kuondokana na utumikishwaji wa watoto kwenye kilimo anasema sababu kubwa ni umaskini kwenye familia ambao husababisha wazazi kutumia watoto wao kufanya kazi kwenye kilimo.
Amesema watoto wanapotumikishwa kwenye kilimo wanashindwa kwenda shule, na hata pale wanapokwenda wanakuwa wamechoka na wanashindwa kusoma ipasavyo kama we... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More