FARU WA SERENGETI KULINDWA KWA VIFAA MAALUMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FARU WA SERENGETI KULINDWA KWA VIFAA MAALUMU


Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha.

Vita dhidi ya ujangili wa Faru, imeendelea kushika kasi na sasa Faru wa serengeti,wataanza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika mradi ambao utagharimu zaidi ya 2.5 bilioni

Mradi huo,unafadiliwa na shirika la uhifadhi za Friedkin conservation Fund(FCF) kwa kushirikiana na shirika la Frunkfurt zoological society na kusimamiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini(TANAPA) na taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI).Mratibu wa Mradi wa uhifadhi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Philbert Ngoti alisema, vifaa hivyo ambavyo vitawezesha Faru wa Serengeti kuwa salama zaidi.

Alisema Faru wa Serengeti wanafungwa vifaa vya aina mbili,vya kielekroniki VHF transmitter ambacho kinawezesha kuwafatilia walipo kila siku na pia wanafungwa katika mguu wa kulia kifaa cha kisasa cha LoRa collar ambacho pia kinafatilia na kuonesha mienendo yao kila siku.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga, alisema zoezi la ufung... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More