FARU WAWEKEWA ULINZI KWA KUFUNGWA VIFAA VYA UTAMBUZI NA LUSUNGU HELELA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FARU WAWEKEWA ULINZI KWA KUFUNGWA VIFAA VYA UTAMBUZI NA LUSUNGU HELELA

Na Lusungu HelelaNaibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya Kisasa, Maafisa wanyamapori watakuwa na uwezo wa kuwaona faru popote walipo wakati wakiwa wamekaa ofisini hali itakayosaidia kuwalinda wanyamapori hao ambao wapo hatarini kutoweka .  Pia amesema Maofisa hao watakuwa na uwezo wa kufuatilia mienendo ya wanyama hao pale walipo na popote wanapoenda ili kujua kama wanaumwa au wanatatizo lolote hali itakayosaidia kwenda kutoa huduma ili wanyama hao waendelee kuishi.  Mhe. Hasunga amezungumza hayo alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mara baada ya kushuhudia zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo.  Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwenye uhifadhi wa wanyamapori hali itakayopelekea majangili kukamatwa hata kabla hawajamuua faru.  Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa faru katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Phillibert Ngoti amem... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More