FEI TOTO ALIYETAMBULISHWA SINGIDA UNITED ASUBUHI, JIONI HII AIBUKIA YANGA NAKO KASAINI MIAKA MITATU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FEI TOTO ALIYETAMBULISHWA SINGIDA UNITED ASUBUHI, JIONI HII AIBUKIA YANGA NAKO KASAINI MIAKA MITATU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye mchana wa leo ametambulishwa na Singida United – jioni hii ametangazwa Yanga kwamba amejiunga na kwa mkataba wa miaka mitatu.
Fei alikuwepo makao makuu ya klabu ya Yanga akiwa na jezi ya klabu huyo na kutambulishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika kama mchezaji mpya wa klabu hiyo pamoja na kiungo mwingine, Jaffar Mohammed kutoka Maji Maji ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
Feisal hakutaka kuzungumza chochote kuhusu kuonekana anatambulishwa na Singida United, lakini Meneja wa JKU, Mohammed Kombo aliyekuwapo mkutanoni pia amesema kwamba Yanga imekamilisha taratibu za kumchukua mchezaji huyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika (katikati) akiwa na wachezaji wapyam Feisal Salum (kushoto) na Jaffar Mohammed (kulia) 

Feisal Salum (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika

Mapema leo, Singida United imemtambulisha Fei Toto kwa kutoa p... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More