FEI TOTO AWAAHIDI YANGA UBINGWA, AOMBA APANGWE MECHI NA SIMBA SEPTEMBA 30 AWAONYESHE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FEI TOTO AWAAHIDI YANGA UBINGWA, AOMBA APANGWE MECHI NA SIMBA SEPTEMBA 30 AWAONYESHE

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KIUNGO chipukizi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewaahidi mashabiki wa klabu yake, Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/2019.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Feisal amesema kwamba pamoja na kwamba mashabiki wa timu hiyo hawaipi nafasi yao kutamba mbele ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC lakini mwishoni mwa msimu watafurahi na roho zao.
Feisal aliyetakata katika mchezo wa kirafiki jana dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Yanga ikiibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee Yussuf Mhilu dakika ya 84 amesema kwamba anajisikia vizuri sana pale anapoona kila anapopata mpira na kuucheza mashabiki wanashangalia, hivyo ahadi yake kubwa ni kuhakikisha anawapa ubingwa msimu huu.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ (kulia) amewaahidi Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

"Ninajua mashabiki wa Yanga wanafurahia ninachokifanya na wana imani kubwa juu yangu. Na mimi ninafurahia hilo na pia najisikia vizuri. kikubwa ninachowaahidi ni ub... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More