FIFA YAMFUNGIA KALUSHA BWALYA MIAKA MIWILI KWA KASHFA YA RUSHWA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FIFA YAMFUNGIA KALUSHA BWALYA MIAKA MIWILI KWA KASHFA YA RUSHWA

KATIKA kile kinachoonekana ni kuendelea kujisafisha, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limemfungia miaka miwili Mjumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Kalusha Bwalya tuhuma za rushwa.
Mwanasoka huyo bora wa zamani wa Afrika, ambaye kwa sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Zambia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CAF, amesimamishwa kujihusisha na shughuli za soka kwa miaka miwili na Kamati ya Maadili ya Kimataifa. 
Katika taarifa yake, barua imesema kwamba uamuzi huo umefuatia uchunguzi uliofanyika juu ya fedha alizopewa Bwalya na Mohammed Bin Hammam, Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Asia na aliyekuwa mgombea Urais wa FIFA. 

Kalusha Bwalya (kushoto) amefungiwa kwa miaka miwili kutojihusisha na soka 

Adhabu hiyo inayoanza mara moja, inaambatana faini ya faranga za Uswisi 100,000 ambazo lazima zilipwe na kiongozi huyo wa Zambia.... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More