Filamu ya Uwoya, Red Light kuonyeshwa kesho Ijumaa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Filamu ya Uwoya, Red Light kuonyeshwa kesho Ijumaa


Baada ya uzinduzi wa Msimu wa Siku kuu na promosheni kutoka kwa Kampuni ya Star Media (T) Ltd, ambapo walitangaza rasmi nia yao ya kuisadia Bongo Movie kwa kununua filamu kadhaa na kuzionyesha kupitia chaneli yao ya Kiswahili, sasa filamu hizo zinaanza kuruka katika chaneli hiyo ya Kiswahili.Ili kurejesha ladha ya filamu za nyumbani maarufu kama Bongo Movie, ambayo kwa muda mrefu watazamaji wameikosa. Msimu huu wa Siku kuu StarTimes wataonyesha jumla ya filamu 25 katika kipindi cha mwezi mzima wa Disemba.Kwa wiki hii ya kwanza ya mwezi Disemba miongoni mwa filamu zitakazoonekana kupitia chaneli ya StarTimes Swahili ni Red light ambayo imemshirikisha mlimbwende Irene Uwoya ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini. Filamu hiyo inamuelezea kijana wa miaka 27 ambaye baba yake aliuwawa na rafiki yake huku mkewe akipona, kisa kikiwa ni pete ya utajiri. Mama na kijana wake wanaamua kuhama mji na kwenda kuishi sehemu nyingine ambako wanakutana na kijana anayewapatia habari kuhusu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More