Fred Aelezea Hisia Zake Kwa Mimi Mars. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Fred Aelezea Hisia Zake Kwa Mimi Mars.

Msanii aliyewahi kuunda kundi la Makomandoo Fred Wayne amefunguka na kusema wazi kuwa katika wasanii wa kike bongo anaowakubali basi hawezi kumuacha kumtaja Mimi  Mars kama msanii wa kwanza.


Fred Wayne amesema kuwa pamoja na kwamba hajawahi kukaa au kupata bahati ya kuongea nakufanya kazi na mwanadada huyo kwa karibu lakini siku zote anatamansana dada huyo ajue kuwa yeye ndio msanii wa kike anaemkubali Tanzania.


Mimi Mars ni moja ya wasanii kutoka Mdee Music , ambapo ni ndugu wa damu wa mwanadada vanesa mdee familia mabayo kwa sasa wanafanya vizuri sana katika swala zima la muziki ingawa kila mmoja ana utofauti wake katika kipaji chake cha uimbaji .


kwa upande wa Fred Wayne kwa sasa anafanya kazi zake kwa kujitegemea mwenyewe tangu kulipovunjika kwa kundi lao la Makomandoo na kuamua kila mmoja kufanya kazi peke yake.


The post Fred Aelezea Hisia Zake Kwa Mimi Mars. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More