Fredy Lowassa kurithi mikoba ya baba yake Monduli kwa Tiketi ya CHADEMA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Fredy Lowassa kurithi mikoba ya baba yake Monduli kwa Tiketi ya CHADEMA


Baada ya kuwepo kwa mashinikizo mbalimbali yakimtaka mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya nne, Edward Lowassa kugombea Ubunge jimbo la Monduli Fred Lowassa, hatimaye ameweza kutimiza maagizo hayo kwa kuchukua fomu rasmi jana Agosti 09, 2018.
Fred Lowassa amechukua maamuzi hayo baada ya jimbo hilo kuwepo wazi kutokana na aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo Julius Kalanga kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.
Mbali na Fred kuchukua fomu hiyo kutoka CHADEMA pia wamejitokeza wanachama wengine ndani ya chama hicho kuonesha nia ya kuomba ridhaa ya Jimbo hilo ambapo ni pamoja na Mwenyekiti Baraza la Wanawake wa CHADEMA mkoa Cecilia Ndosi, diwani viti maalum, Yona Laizer, Lobulu Kivuyo aliwahi kuwa mgombea katika uchaguzi mdogo uliopita Kata ya Muhita na Eric Ngwijo.
Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Aman Golugwa amesema wagombea hao wanatarajiwa kupigwa kura za maoni katika kikao kitakachofanyika Agosti 12, 2018 siku ya Juma... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More