FUKWE KUIMARISHWA NA KUWA KIVUTIO CHA UTALII-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

FUKWE KUIMARISHWA NA KUWA KIVUTIO CHA UTALII-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaweka mikakati madhubuti kwa lengo la kuimarisha matumizi ya fukwe kama sehemu ya kivutio cha utalii ili kongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini na kutengeneza ajira kwa wananchi sambamaba na kukuza uchumi wa Taifa.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 12, 2018) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye ufunguzi wa onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili International Tourism Expo, katika  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar ES Salaam.
Onesho hilo linalofanyika kwa siku tatu nchini linahudhuriwa na wafanyabishara wakubwa wa utalii takriban 170  kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na wauzaji wa bidhaa za utalii takriban 300 kutoka ndani na nje ya nchi.
Waziri Mkuu amesema sekta ya utalii nchini inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na takriban ajira 1,500,000, ambapo kati ya ajira zote za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja.
Amesema kutokana na juhudi za utangazaj... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More