GARI LA MBUNGE LAUA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GARI LA MBUNGE LAUA

Gari la Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T 348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro amepoteza maisha papo hapo.
Ajali hiyo imetoka leo Agosti 9 ambapo ndani ya gari hiyo alikuwepo dereva mwenyewe kwani alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar es Salaam.
Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More