Gari la Mbunge wa CHADEMA lashambuliwa kwa risasi, Mawakala wao watolewa nje kwenye vituo vya uchaguzi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Gari la Mbunge wa CHADEMA lashambuliwa kwa risasi, Mawakala wao watolewa nje kwenye vituo vya uchaguzi

Gari la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Mhe. Anna Gidarya limeshambuliwa kwa kupigwa risasi kwenye matairi ya mbele na nyuma ya ubavu mmoja muda mfupi uliopita akiwa katika kata ya Majengo, Monduli mkoani Arusha.


Taarifa zilizotolewa na chama hicho, zimeeleza kuwa gari hiyo imeshambuliwa leo asubuhi, hata hivyo haijulikani ni watu gani walioshambulia gari hilo.


Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi, amesema hana taarifa juu ya tukio hilo, anachojua ni kuwa kwa sasa hali ya uchaguzi wilayani Monduli ipo safi.


Wakati hilo likitokea, Mawakala wa CHADEMA kata ya Esilalei wote wametolewa nje kwa kukosa fomu za kiapo. Tazama video wakiongea hapa chini


Leo Septemba 16, 2018 ni siku ya marudio ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga na Monduli, ambapo wananchi wa majimbo hayo wanapiga kura kuchagua madiwani na wabunge.


The post Gari la Mbunge wa CHADEMA lashambuliwa kwa risasi, Mawakala wao watolewa nje kwenye vituo vya uchaguzi appeared first on Bongo5... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More