GAVANA SHILATU ALIA NA KANDARASI ZA UJENZI TARAFA YA MIHAMBWE WILAYANI TANDAHIMBA, MTWARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GAVANA SHILATU ALIA NA KANDARASI ZA UJENZI TARAFA YA MIHAMBWE WILAYANI TANDAHIMBA, MTWARA

Wakandarasi wanaoshinda kandarasi za ujenzi wametakiwa kuacha urasimu na  ubabaishaji  kwenye utekekezaji wa kazi wanazolipwa na Serikali  na miradi yote itakayokosa ubora wa viwango isipokelewe.
Pia imeelezwa kwamba  si busara kwa kampuni za ujenzi  zilizopitishwa chini ya taratibu za kisheria, kushinda zabuni na kulipwa fedha  za umma zishindwe kujenga kwa viwango na kumaliza kwa wakati. 
Msimamo huo umetolewa na Afisa Tarafa Mihambwe Wilayani Tandahimba mkoa wa Mtwara Gavana Emmanuel Shilatu  alipokagua ujenzi miradi ya ofisi, soko na choo  katika kiijiji cha Ngongolo  kata ya Miuta. Alisema Wakandarasi wana wajibu wa kutimiza ahadi kama mikataba yao ilivyoeleza, kujenga majengo kumaliza kwa wakati husika kazi zao bila visingizio vyovyote.
"Tabia za uzembe na ubabaishaji mkubwa wa ujenzi chini ya kiwango na miradi mingine kutokuanza kabisa licha ya Mkandarasi kupewa pesa tangu Septemba 2018 inatakiwa ife.
"Ifike mahali  uzalendo utusute na kuona aibu. Tuheshimu fedha za umma ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More