GAVANA SHILATU ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GAVANA SHILATU ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA


Na Mwandishi wetu Mihambwe 
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu Leo Jumamosi Juni 15, 2019 ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira akishirikiana na viongozi pamoja na Wananchi wa kata ya Kitama. 
Gavana Shilatu aliwasihi Wananchi wote kuhakikisha wanasafisha na kuyatunza mazingira ili nayo yawatunze ikiwemo kila iitwapo jumamosi kuwa ni siku ya usafi wa mazingira. 
*”Nimetoa maelekezo kwa Watendaji kata na Vijiji kuhakikisha kila iitwapo jumamosi ndani ya Tarafa ya Mihambwe wanashiriki na kusimamia zoezi la kitaifa la usafi wa mazingira na wakati wote wanahakikisha maeneo yao ni safi. Nami nimekuja hapa kuonyesha kwa vitendo kwamba suala la usafi wa mazingira ni jukumu letu sote.”* Alisema Gavana Shilatu. 
Usafi wa mazingira wa kila jumamosi ni agizo na kampeni ya kitaifa ambayo kila Mtu anapaswa kuitii kwa kufanya usafi na kuyatunza mazingira yawe safi nyakati zote. 
Katika zoezi hilo la usafi wa mazingira Gavana Shilatu aliambata na Waten... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More