GENK YA SAMATTA YAANZA KUPUNGUA UTAMU, YACHAPWA MECHI YA PILI MFULULIZO YA LIGI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GENK YA SAMATTA YAANZA KUPUNGUA UTAMU, YACHAPWA MECHI YA PILI MFULULIZO YA LIGI

Na Mwandishi Wetu, GENK
MABINGWA watetezi, KRC Genk jana wamepoteza mechi ya pili mfululizo ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji baada ya kuchapwa 2-0 nyumbani na Zulte-Waregem Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mfungaji bora wa timu msimu uliopita, Mbwana Samatta alicheza kwa dakika zote 90 jana lakini kwa mara nyingine akashindwa kufunga.
Mabao yaliyoizamisha Genk jana yalifungwa na washambuliaji Mnorway, Henrik Rorvik Bjordal dakika ya sita na Mrundi, Saido Berahino dakika ya 78.

Mbwana Samatta akimtoka beki wa Zulte-Waregem usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk

Mechi ya kwanza ya Ligi, Genk ilichapwa 3-1 na wenyeji, KV Mechelen Agoti 3 Uwanja wa AFAS- Achter de Kazerne mjini Mechelen, Malines siku ambayo Samatta alifunga bao lake la kwanza la msimu dakika ya dakika ya 45 na ushei akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen. 
Na hilo lilikuwa bao la kusawazisha baada ya KV Mechelen kutangulia kwa bao la Muivory Coast, William Togu... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More