GESI ASILIA KUTUMIKA MAJUMBANI MKOANI MTWARA – KALEMANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GESI ASILIA KUTUMIKA MAJUMBANI MKOANI MTWARA – KALEMANI


Na Rhoda James- Mtwara

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jana tarehe 10 Agosti, 2018 amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kusambaza Gesi Asilia majumbani mkoani Mtwara. Waziri Kalemani, amefanya zoezi hilo leo katika shule ya Ufundi ya Mtwara mara baada ya kuzidua MW4 za umeme katika kituo cha Umeme cha Mtwara.

Waziri Kalemani alisema kuwa, ujenzi wa mtambo huu umegharimu jumla ya billioni 1.5 kwa ajili ya kuwapelekea watumiaji wa awali wasiopungua 150 ambao bada ya miezi mitatu wataanza kutumia gesi hiyo majumbani. Aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia ni madogo sana yaani ni kama hayapo, kwa kuwa wananchi wengi wanatumia kuni na mkaa kwa wengi kuliko gesi.

“Sasa mtugi wa gesi ni takriban shilingi 55,000/- lakini ukitumia gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani itakuwa shilingi 25,000/- na utatumia kwa mwezi mzima hivyo ni nafuu kwa mwananchi wa Tanzania,” alisema Wazari Kalemani.

Mwezi mei... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More