Goli ambalo Abdi Kassim hatolisahau maisha yake yote - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Goli ambalo Abdi Kassim hatolisahau maisha yake yote

Abdi Kassim ‘Babi’ ameandika historia ya aina yake kwenye soka la Tanzania. Jina lake litaendelea kudumu kwenye vitabu vya historia vya soka la Bongo.


Babi ndiye mfungaji wa bao la kwanza kwenye uwanja mpya wa Taifa wakati ukizinduliwa rasmi kuanza kutumika Septemba Mosi, 2007.


Kiungo huyo alifunga bao hilo katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na Uganda ‘The Cranes’, Stars ilishinda 1-0.


Babi alifunga bao hilo kipindi cha pili kwa shuti kali la mguu wake wa kushoto kwa umbali unaokadiriwa kuwa mita 35.


“Nakumbuka pasi alinipa Haruna Moshi ‘Boban’ nilituliza mpira na kuusogeza kidogo na kupiga shuti kali ambalo lilimshinda kipa kudaka.”


Babi anasema alifunga goli hilo upande wa goli la Kusini la ueanja wa Taifa, upande ambao mashabiki wa Yanga wanapendelea kukaa.


Hilo ni goli ambalo linaendelea kuwa bora kwenye maisha ya soka ya Babi kutokana na historia iliyobebwa na goli hilo.


Full video unaweza kuiangalia kwa kirefu zaidi #YouTube kupitia #DaudaTV... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More