Gongo yaua Mwalimu mkoani Ruvuma, Yadaiwa alikunywa akiwa na njaa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Gongo yaua Mwalimu mkoani Ruvuma, Yadaiwa alikunywa akiwa na njaa

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, Hekima Gregory maarufu (49), amefariki Dunia baada ya kunywa pombe haramu aina ya gongo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa amesema taarifa ya tukio hilo ilitolewa kwenye kituo cha Polisi cha Matemanga kutoka kwa Mratibu Elimu Kata ya Matemanga, Rashidi Nasoro.


Kamanda Marwa amesema katika taarifa hiyo Nasoro alieleza kuwa Mwalimu Gregory alikutwa akiwa anakunywa pombe haramu ya gongo na inadaiwa kuwa alikuwa hajapata chakula.


Imeelezwa kuwa hatua ya kwanza iliyochukuliwa, Mwalimu huyo alipelekwa katika hospitali ya misheni ya Kiuma ambako alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.


Chanzo: Nipashe


The post Gongo yaua Mwalimu mkoani Ruvuma, Yadaiwa alikunywa akiwa na njaa appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More