GOR MAHIA ATWAA KOMBE LA SPORTPESA SUPERCUP, KUKIPIGA NA EVERTON GODSON PARK - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GOR MAHIA ATWAA KOMBE LA SPORTPESA SUPERCUP, KUKIPIGA NA EVERTON GODSON PARK

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Klabu ya Soka ya Gor Mahia ya nchini Kenya imeendeleza ubabe wake kwa kunyakua kombe la Sportpesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Simba ya Tanzania kwa goli 2-0 katika Uwanja wa Afraha Kwenye Jiji la Nakuru nchini Kenya
Kombe la Sportpesa Super Cup lilianzishwa mwaka jana 2017 na kufanyika nchini Tanzania ambapo Gor Mahia wajulikanao kama K'Ogalo kuwafunga mashemeji zao Fc Leopard.
 Gor Mahia  walioanza kwa kasi toka kwenye mchezo wa kwanza waliweza kutimia dakika 5 kuweza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaje wake Meddi Kagere ambapo iliwapelekea Simba kutafuta goli la kusawazisha ila mpaka mapumziko matokeo yalisalia 1-0.Kipindi cha pili kilianza na katika dakika ya  62 Mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge aliweza kuiandikia timu yake goli la pili na la ushindi na kupoteza matumaini ya Simba kunyakua ubingwa huo.
Gor Mahia na Simba zinakutana baada ya miaka 37 ambapo Simba wakipambana na aliyekuwa Kocha wao wa zamani wa Simba Dylan Kerr akiwa Kocha mkuu wa timu hiyo.
Baada ya ushindi huo Gor Mahia wamefanikiwa kuondoka na fedha kiasi cha Dola 30,000, kombe na kwenda kucheza mchezo na timu ya Everton nchini Uingereza huku Simba akinyakua dola 10,000.
Nayo Singida imefanikiwa kushika nafasi ya tatu akiifunga Kakamega goli 4-1.Gor Mahia XI: Shaban Odhoji, Philemon Otieno, Godfrey Walusimbi, Haron Shakava, Joash Onyango, Ernest Wendo, Humphrey Mieno, George Odhiambo, Francis Kahata, Jacques Tuyisenge and Meddie Kagere.
Simba XI: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Yusuf Mlipili,  Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Jonas Mukude, Shiza Kichuya, Yasin Muzamiru, Rashid Mohamed, Juma Rashi and Adam Salamba.


Source: Issa MichuziRead More