GWIJI WA SIMBA SC, MTEMI RAMADHANI ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UENYEKITI WA KLABU NOVEMBA 3 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

GWIJI WA SIMBA SC, MTEMI RAMADHANI ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UENYEKITI WA KLABU NOVEMBA 3

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa zamani wa Simba SC, Mtemi Ramadhani amejitokeza kuwania Uenyekiti wa klabu hiyo kama mmoja wagombea wawili tu wa nafasi hiyo, mwingine Swedi Nkwabi.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania ana uzoefu mkubwa wa uongozi wa soka, baada ya kupitia kwenye nafasi mbalimbali, lakini nyingi za kuteuliwa.
Ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya viongozi tofauti na mara ya mwisho alikuwepo chini ya Rais Leodegar Chillah Tenga, mchezaji mwenzake wa zamani wa Taifa Stars.
Jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kuchukua fomu na orodha kamili ya wagombea waliojitokeza ni 21 kwa nafasi zote, wawili wa Uenyekiti, wawili wa Ujumbe kwa Wanawake na 17 kwa Wajumbe wa Bodi.

Mtemi Ramadhani (kushoto) akiwa nyota wa sasa klabu ya Simba, Shiza Kichuya

Nafasi za Wajumbe wa Wanawake waliojitokeza ni Jasmin Badar Soud na Asha Ramadhani Baraka, wakati Wajumbe wa Bodi ni Hussein Kitta Mlinga, Iddi Noor Kajuna, Dk. Zawadi Ally Kadu... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More