HABIB KIYOMBO KUWAKUTANISHA MEZANI SINGIDA UNITED NA MAMELODI SUNDOWNS - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HABIB KIYOMBO KUWAKUTANISHA MEZANI SINGIDA UNITED NA MAMELODI SUNDOWNS

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
KLABU ya Singida United inatarajiwa kufanya mazungumzo na Mamelodi Sundowns ya Afrika juu ya mshambuliaji chipukizi, Habib Hajji Kiyombo. 
Kiyombo amerejea nchini jana kutoka Afrika Kusini baada ya karibu mwezi mzima wa na mabingwa wa zamani wa Afrika, Mamelodi kwa majaribio.
Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba Mamelodi imevutiwa na mchezaji huyo na inamuhitaji ahamishie huduma zake Afrika Kusini.
Sanga amesema kwamba Kiyombo alipokuwa Afrika Kusini alianzia majaribio yake katika timu ya vijana kwa siku 10 ambako alipoonyesha uwezo akapandishwa kikosi cha kwanza kwa siku 10 nyingine, ambako pia alifanya vizuri.
Sanga Festo (kulia) akiwa na Habib Kiyombo wakati wanamsajili kijana huyo Juni mwaka huu

“Wamependezewa na huduma ya mchezaji, wamependezewa na umri alionao, lakini pia kwa kiwango alichonacho, nidhamu na vile ambavyo amevionyesha uwanjani wamefurahishwa sana na Habib Kiyombo. Na... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More