Haji Manara ajitwisha mzigo wa kocha wa Simba SC ‘Kwa matokeo haya nipo tayari kuwajibishwa’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Haji Manara ajitwisha mzigo wa kocha wa Simba SC ‘Kwa matokeo haya nipo tayari kuwajibishwa’

Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema yupo tayari kuwajibishwa kufuatia timu yake kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.Manara amesema kwanza anaomba radhi kwa mashabiki wa Simba SC, Na kudai kuwa matokeo hayo ni fedheha kubwa klabu hiyo.


Am Sorry Guys 🙏 Hakika huu ni msiba na ni fedheha kuu. Nipo tayari kuwajibika kwa matokeo haya, Nawaomba tena Samahani Washabiki wetu.“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Hata hivyo, Mwenye kubeba jukumu la kiufundi ndani ya klabu yoyote ile ni Kocha Mkuu na Benchi lake la ufundi na sio jukumu la msemaji wa klabu.


Leo Klabu ya Simba imetupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Kwa kutoka sare ya 1-1 na klabu ya UD Songo kutoka Msumbiji.


Soma zaidi : http://bongo5.com/breaking-simba-sc-watupwa-nje-michuano-ya-klabu-bingwa-afrika-yaungana-na-vijana-wa-kinondoni-kmc-08-2019/


 


The post Haji Manara ajitwisha mzigo wa kocha wa Simba SC ‘Kwa matokeo haya nipo tayari kuwajibishwa’ app... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More