HAKUNA UPENDELEO NAFASI ZA JKT ARUMERU - DC JERRY MURO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HAKUNA UPENDELEO NAFASI ZA JKT ARUMERU - DC JERRY MURO

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewahakikishia mamia ya vijana waliojitokeza katika usahili wa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwa usahili utafanyika kwa Uwazi na Ukweli na kusisitiza kuwa hapatakuwa na upendeleo zaidi ya kufuata Sheria pmoja na  sifa zinazotakiwa kwa vijana kujiunga na jeshi.Aliyasema hayo leo ofisini kwakwe  wakati akiongea na Vijana waliojitokeza kwa wingi kuomba nafasi za kuingia katika mafunzo ya JKT ambapo kwa sasa usahili wa kuandikisha vijana hao kwa wilaya ya Arumeru unaendelea. DC Muro alibainisha kuwa wao kama watachagua vijana wote wenye sifa ya kujiunga na jeshi hilo na hawatamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa anawadanganya Vijana hao kuwa watoe ela ndio wapate nafasi "Wapo watu wanaopita uko barabarani wakiomba hela  huku wakiwa wanajinadi kwa kuwalaghai vijana hawa kuwa wanauwezo wakuwapa nafasi kitu ambacho sio chakweli hivyo kueni makini na msikubali kudanganywa mkatoa fedha zebu, nanapenda... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More