HALMASHAURI WILAYA YA KALIUA, WADAU WA MAENDELEO WAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HALMASHAURI WILAYA YA KALIUA, WADAU WA MAENDELEO WAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI

Na Editha Shija, Tabora

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wilayani humo wamejipanga kumaliza kero ya maji kwa wananchi ambayo imekuwa ya muda mrefu katika maeneo karibu yote wilayani humo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dk.John Pima alibainisha kuwa ushirikiano mzuri wa watendaji na wataalamu wa halmashauri umechochea kasi nzuri ya ukusanyaji mapato, hivyo kumewezesha miradi mingi ya maji kutekelezwa kwa asilimia 100.

Amesema kuwa mfuko wa programu ya maji umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo na wana uhakika katika kipindi kifupi kijacho tatizo la maji litapungua kwa kiasi kikubwa kama si kumalizka kabisa.Pima ameongeza kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya upatikanaji maji , ametaja miradi ya maji iliyotekelezwa kwa asilimia zote ni ujenzi wa mantenki mawili ya kuvunia maji mvua yenye ujazo wa lita 50,000 yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More