HALMASHAURI YA BUHIGWE, OFISI YA MBUNGE WAANDAA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HALMASHAURI YA BUHIGWE, OFISI YA MBUNGE WAANDAA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
HALMASHAURI ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wameandaa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo wilayani humo.
Lengo ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuongeza uelewa kwa wajasiriamali katika shughuli wanazofanya.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo jana wilayani Buhigwe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Anosta Nyamoga amesema semina hiyo inamalengo matatu , moja ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ili kuwawezesha na kuwapa mafunzo wajasiriamali wadogo wadogo.
Pia kuongeza mapato kwa halmashauri kwakuwa wajasiriamali wakiongeza kipato hata pato la halmashauri linaongezeka kupitia ukusanyaji wa kodi na kuboresha maisha ya wananchi.
Amesema asilimia kubwa ya mapato ya Wilaya ya Buhigwe yanategemea ukusanyaji wa ushuru wa mazao na kodi kutoka kwa wajasiriamali wadogo , semina hiyo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali na kufaungua masoko ya nje ya nchi kwa kuwajenga wananchi kutengeneza bidhaa zenye ubora na kutumia masoko ya ujirani mwema kuuza bidhaa zao na kuongeza kipato chao itasaidia uchumi kuongezeka.
Amesema kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 walikusanya shilingi milioni 450 , na kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wamekusanya milioni 550 na Malengo ya Wilaya hiyo ni kufikia kukusanya kiasi cha Sh bilioni moja ifikapo 2020 kutokana na Miundombinu ya biashara kuboresha na kukamilika kwa soko la ujirani mwa litakalo jengwa Manyovu, ambapo wanatarajia kukusanya zaidi ya milioni 100 kupitia soko hilo.
" Wilaya ya Buhigwe tumejipanga ipasavyo kuhakikisha Wananchi wetu wanatoka kwenye maisha waliyokuwa nayo ya kufanya biashara kwaajili ya kupata chakula kwa sasa tunataka waanze kufanya biashara kwa malengo zaidi kwakuwa fursa ni nyingi na Wananchi walikuwa hawazitumii tunaamini kupitia semina hii uchumi utaongezeka na manufaa watayaona", alisema mkurugenzi huyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>>>
Baadhi ya Wajasiriamali Wadogo wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini humo mapema jana,mafunzo hayo yaliandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Manyovu .Lengo la mafunzo hayo ikiwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuongeza uelewa kwa wajasiriamali katika shughuli wanazofanya.


Source: Issa MichuziRead More