Halmashauri Zatakiwa Kutenga Maeneo ya Kilimo kwa Vijana - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Halmashauri Zatakiwa Kutenga Maeneo ya Kilimo kwa Vijana

Na. Georgina Misama - MAELEZO
Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya Vijana kuyatumia katika shughuli za kilimo.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhisho ya siku ya Vijana Duniani.
Mavunde alisema hadi hivi sasa Serikali imetenga takribani hekta laki mbili katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwapa vijana fursa ya kuyatumia katika shughuli za kilimo."Nazitaka Halmashauri zote nchini ambazo bado hazijatenga maeneo hayo, kufanya hivyo ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka 2018 inayosema 'Mazingira salama kwa Vijana' ambapo serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira hayo kwa vijana." alisema Mavunde.
Akiongelea kuhusu mwitikio wa vijana kwenye shughuli za kilimo, Mavunde alisema kuwa vijana wengi wameanza kujishughulisha katika kilimo na ipo mifano mingi hai ya vijana walioamua kujiajiri kwenye kilimo biashara kama SUGEKO na wanafanya vi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More