Halotel kuwazawadia wateja wake maadhimisho ya miaka 3 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Halotel kuwazawadia wateja wake maadhimisho ya miaka 3

- Wateja kupata fursa kutoa mawazo kuboresha huduma.

Ikiwa katika shamrashamra ya kuadhimisha miaka 3 ya utoaji wa huduma kwa watanzania, Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imetangaza mpango wa kutoa huduma ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja.

Mpango huo uliopewa jina la “LONGA TUSONGE” pamoja na faida zingine una lengo la kuwashirikisha wateja wote pamoja na wafanyakazi wa Halotel katika kufanya maboresho ya utoaji huduma mbalimbali kupitia mawazo yao wakati huu ambapo kampuni hiyo inapoadhimisha miaka mitatu ya utoaji huduma zake za Mawasiliano hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, mkakati huo ni sehemu ya kuthamini mchango mkubwa wanaoutoa wateja wake tangu kuanza kutolewa kwa huduma kupitia mtandao huo hapa nchini .

Amesema tangu kuingia kwa huduma za... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More