Hamisa Mobeto na Zamaradi Hapatoshi. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Hamisa Mobeto na Zamaradi Hapatoshi.

Mwanadada Hamisa Mobeto na mwanamama Zamaradi Mketema wameingia katika bifu zito na kujibishana  maneno katika mitandao ya kijamii baada ya Zamaradi kumshushia maneno mazito hamisa Mobeto kwa kumsambazia habari za uongo kuhusu makubaliana yao ya kushonewa nguo kwa ajili ya 40 ya mtoto wa Zamaradi.


Katika kurasa za udaku , hapo awali kuna ukurasa uliandika mambo mengi kuhusu zamaradi ikiwa ni pamoja na kwamba nguo alivaa siku ya sherehe hiyo ilitakiwa kushonwa kwa hamisa lakini cha ajabu baada ya hamisa kumpa mshono zamaradi, basi zamaradi akakimbia kwa fundi mwingine , lakini pia kuwa sherehe hiyo ilichangishwa pesa kutokwa kwa wadau na mshabiki zake .


Baada ya maneno hayo ndipo Zamaradi naeo alipoamka na kutaka kuonyesha ushahidi wa yote yaliyokuwa yakiongelewa na kusema kuwa pesa hakuwahi kumchangisha mtu yoyote zaidi ya pesa ya zawadi ambayo wanakikundi waliamua kumpa siku hiyo na wala hakuwa anajua hilo.”tukija kwenye nguo naambiwa kuwa nilipewa mshono na mwingine na nikaenda kushona kwa mwigine, funny nimeattach hapo juu na picha muone kuwa mimi ndio nilietuma mshono wake na wala sio yeye.kutokana na kupishana na muda nikaona bora nikashone kwingine , kwanza ni uamuzi wangu kuamua kushona popote pale.”


Hata baada ya zamaradi kuongea hivyo, Hamisa nae aliamua kuja na kuongea  nakuweka picha za chat  zinazoonyesha mazungumzo yake na zamaradi na kwa jinsi gani mwanamama huyo alimtafuta na kuomba ushauri wa nini cha kushona siku hiyo.


 


 


The post Hamisa Mobeto na Zamaradi Hapatoshi. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More