Hans Cana Afurahishwa na Kutimia kwa Ndoto Yake ya Kufanya Kazi na Msanii Huyu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Hans Cana Afurahishwa na Kutimia kwa Ndoto Yake ya Kufanya Kazi na Msanii Huyu

Muongozaji wa video za muziki nchini, Hanscana amefunguka na kudai ametimiza miongoni mwa ndoto zake alizokuwa nazo maishani mwake, baada ya kufanikiwa kufanya kazi na mnenguaji wa dansi Luiza Mbutu ambaye amekuwa anamfuatilia tangu alipokuwa mtoto.


Hanscana amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye eNewz inayorushwa na EATV, na kusema licha ya kuwa amebahatika kufanya kazi na mkongwe huyo wa dansi lakini haikuwa rahisi kwa yeye kurekodi nyimbo yenye mahadhi ya dansi kutokana na watu waliokuwa wanamzunguka ni bongo fleva.


“Nimepata ugumu sana katika ku-shoot video yake maana watu walikuwa wengi hadi muda mwingine unaweza kujikuta mtu mmoja ameimba mara mbili. Ilikuwa inanichanganya sana kwasababu sijawahi ku-shoot watu wengi kiasi hicho”, amesema Hanscana.


Pamoja na hayo, Hanscana ameendelea kwa kusema “nimem-charge ‘normal’ kwa sababu ilikuwa ndoto yangu kufanya naye kazi Luiza Mbutu. Kwa mara ya kwanza namsikia huyu mama nilikuwa bado nasoma shule ya msingi. Luiza ni miongoni mwa wanamuziki mama yangu anaowakubali”.


Kwa upande mwingine, Hanscana amewashauri wasanii wa kiume wa bongo fleva kumtumia vizuri Luiza Mbutu katika nyimbo zao pale wanapohitaji wasanii wa kike kwa madai dada huyo anasauti nzuri ya kuimba pamoja na kujua kucheza


The post Hans Cana Afurahishwa na Kutimia kwa Ndoto Yake ya Kufanya Kazi na Msanii Huyu appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More