HANS MABENA KUCHEZESHA MECHI YA WATANI, SIMBA NA YANGA JUMAMOSI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HANS MABENA KUCHEZESHA MECHI YA WATANI, SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa mahasimu wa jadi, Yanga SC na Simba SC utakaofanyika Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam utachezeshwa na refa Hans Mabena kutoka Tanga.
Bodi ya Ligi Tanzania (TLB) imetaja marafa watakaotumika kwenye mechi hiyo na Mabena atasaidiwa na washika vibendera Mohammed Mkono na Kassim Mpanga, wakati Heri Sasi atakuwa refa wa akiba.
Watani wa jadi, Simba na Yanga wanakutana Jumamosi katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza Septemba 30, mwaka jana Uwanja wa Taifa.

Hans Mabena (katikati) atachezesha mechi ya watani wa jadi Jumamosi Uwanja wa Taifa

Mchezo wa Jumamosi unakuja wakati Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 58 za mechi 23, ikiizidi pointi tisa Azam FC inayofuatia katika nafasi ya pili, ingawa ina mechi mbili mkononi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 36 za mechi 15.
Viingilio katika mchezo wa Jumamosi vinatarajiwa kuwa Sh. 7,000 kwa mzunguko... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More