HASSAN KESSY ATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HASSAN KESSY ATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, OMDURMAN
BEKI Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy amefuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na timu yake, Nkana FC kufungwa mabao 4-1 na Al-Hilal Omdurman usiku wa jana Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman katika mchezo wa mwisho wa Kundi C.
Mabao ya Al-Hilal yalifungwa na Sharaf Eldin Ali dakika ya tano, Waleed Bakhet Hamid mawiloi dakika ya 19 na 61 na Idris Mbombo dakika ya 77, wakati la Nkana lilifungwa na Walter Bwalya dakika ya 48.
Lakini Hassan Kessy, mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga za Dar es Salaam hakuwepo hata benchi kwenye mchezo wa jana nchini Sudan.

Hassan Kessy (kushoto) amefuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 

Al-Hilal inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake 11, ikifuatiwa na Nkana FC yenye pointi tisa, timu nyingine ya Zambia, ZESCO United imeshika mkia kwa pointi zake pamoja na kuifunga Asante Kotoko 2-1 jana.
Mbali na Al Hilal na Nkana kufuzu Robo Fainali, timu nyingine zilizofuzu ni RSB Berkane na Hass... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More